ARSENAL YAIFUMUA VIBAYA LEICESTER CITY

0 comments
Walcott & Sanchez
Arsenal wameamka kwa mara nyingine tena baada ya kuwafumua vibaya Leicester City kwa mabao 5-2.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Alexis Sanchez ambaye alipiga hat-trick mnamo dakika za 33, 58 na 81 huku Walcott akifunga lake dakika ya 18 na Giroud akifunga dakika ya 90.
Kwa upande wa Leicester magoli yao yalifungwa na Jamie Vardy katika dakika za 13 na 89
Vikosi vilikuwa hivi:
Leicester (4-4-2): Schmeichel, de Laet, Huth, Morgan, Schlupp, Mahrez, Kante, Drinkwater (Kramaric 78), Albrighton (Ulloa 64), Okazaki (King 45), Vardy
Ozil Arsenal
Wachezaji wa akiba wasiotumika: Simpson, Schwarzer, Inler, Dodoo
Kadi: Drinkwater
Mfungaji: Vardy 13, 89 
Arsenal (4-2-3-1): Cech, Bellerín, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Flamini (Arteta 21), Cazorla, Ramsey (Oxlade-Chamberlain 77), Ozil, Sánchez, Walcott (Giroud 80)
Wachezaji wa akiba wasiotumika: Debuchy, Gibbs, Ospina, Chambers 
Kadi: Arteta 
Wafungaji: Walcott 18, Sanchez 33, 57, 81, Giroud 90 
Mwamuzi: Craig Pawson
Mahudhurio: 32,047 
Mchezaji bora wa mchezo: Alexis Sanchez 

Read More »
We need your favorite Opinion! Just give us your Comment below please!

Ikitokea free-kick, Neymar anawaza goli tu ..!! Messi anamchukulia poa?

0 comments
Staa wa Soka Neymar da Silva Santos Júnior ni mkali ambaye anakamilisha kikosi cha watatu wakali wa Barcelona, yani hapo yuko yeye Luis Suárez na Lionel Messi.
Kwenye Timu inaweza ikatokea Mchezaji mmoja anapewa nafasi zaidi ya kupiga mashuti ya penati kama ikitokea, au nafasi ya kupiga faulo.. kuna vitu vinaendelea Uwanjani ambavyo watu wa nje huenda hawajui…
maxresdefault
Nimekuwa napiga sana free-kicks nikiwa na Klabu yangu ya Barcelona na hata kwenye Timu ya Taifa… Huwa napenda nione nafanya vizuri zaidi kila wakati, na kila ikitokea nafasi ya kupiga najiweka tayari kushinda goliNeymar.
Majina ya wakali watatu wa Barcelona yanatambuliks lakini Neymar anasema sio kila mtu anaoewa nafasi ya kupiga free-kicks ikitokea >>>> ‘Sina hofu yoyote kuhusu Messi kupiga free-kicks nyingi zaidi, sisi wote tunajua yeye ni mkali zaidi na mara nyingi anatupa ushindi wa Barcelona… ikitokea akinipa nafasi ya kupiga free-kicks nakuwa tayari wakati wowote, mara nyingi huwa tunajadiliana nani apige lakini mara nyingi Messi anatusaidia‘ >>> Neymar.
Ninacho kipande cha video, unaweza kucheki free-kicks za Neymar kwenye ubora wake kuanzia mwaka 2011 mpaka 2015.


Read More »
We need your favorite Opinion! Just give us your Comment below please!

Manchester City Yapata kipigo cha paka mwizi kutoka kwa Tottenham Hotspur

0 comments
Ligi kuu ya Uingereza Barclays Premier League imeendelea tena jumamosi ya leo tarehe 29, September – mchezo wa kwanza siku ya leo umewakutanisha Manchester City dhidi ya Tottenham Hotspur.
  Mchezo huo uliopigwa katika dimba la White Hart Lane umemalizika kwa City kupata kipigo kizito kutoka kwa Spurs.
Spurs walianza kuliona lango la Spurs katika dakika ya 25 kwa goli lilofungwa na mchezaji mpya City De Bruyne – Spurs wakafanikiwa kusawazisha dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza, goli likifungwa na beki wa pembeni Eric Dier.
  Dakika 5 baada ya mapumziko Spurs wakapata goli la pili lilofungwa na beki wa kati Alderweireld na muda mfupi baadae mfungaji bora wa Spurs msimu uliopita Harry Kane akafungua akaunti yake ya magoli msimu huu kwa kufunga goli la 3.
 
Dakika ya 79 Winga wa kiargentina Eric Lamela akashindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la City kwa kufunga goli la nne.
TIMU ZILIPANGWA HIVI
Tottenham (4-2-3-1): Lloris 7.5, Walker 6, Alderweireld 7, Vertonghen 7, Davies 6, Dier 8, Alli 6, Lamela 7 (Carroll 87), Son Heung-min 6 (N’Jie 75), Eriksen 6.5 (Chadli 68), Kane 7
Subs not used: Rose, Vorm, Trippier, Townsend, Carroll
Booked: Lamela, Dier, Eriksen, Alli, Kane  
Scorers: De Bruyne 25
Manchester City (4-5-1): Caballero 4.5, Sagna 6, Demichelis 5, Otamendi 5.5, Kolarov 5, Fernandinho 6 (Nasri 69), Fernando 6, De Bruyne 6.5, Toure 5.5 (Jesús Navas 56), Sterling 5, Aguero 5 (Roberts 86)
Subs not used: Hart, Zabaleta, Barker, Evans
Booked: Demichelis
Scorers: Dier 45, Alderweireld 50, Kane 61, Lamela 79
Referee: Mark Clattenburg 4.5

Read More »
We need your favorite Opinion! Just give us your Comment below please!

MAMBO MUHIMU AMBAYO LAZIMA UYAJUE KABLA YA MECHI YA SIMBA VS YANGA

0 comments
Simba vs Yanga picLeo ni siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa sana na mashabiki wengi wa soka la Tanzania, leo ndio siku ambayo unapigwa mtanange wa Dar es Salaam Darby (Yanga vs Simba) mechi hii inatajwa kuwa miongoni mwa Derby kubwa barani Afrika lakini ikiwa ni Derby yenye upinzani mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Simba na Yanga zinakutana leo kwenye raundi ya nne ya VPL lakini ikiwa ni mechi ya kwanza inayozikutanisha timu hizo msimu huu, hapa chini nimekuwekea vitu muhimu unavyotakiwa kuvijua kabla ya mechi haijapigwa ili wakati wa mchezo utapofika unakuwa unajua vizuri nini kinaendelea.
Matokeo ya timu zote msimu huu mpaka sasa
Baada ya mechi tatu kuwa zimechezwa hadi sasa, timu zote zimeshinda michezo yote mitatu Simba imeshinda mechi zake dhidi ya African Sports na Mgambo JKT ugenini kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga mechi yao ya tatu walishinda wakiwa kwenye uwanja wa taifa dhidi ya Kagera Sugar. Yanga mechi zao zote wameshinda wakiwa kwenye uwanja wa taifa dhidi ya Coatal Union, Tanzania Prisons na JKT Ruvu.
Vita ya Hamisi Kiiza vs Amis Tambwe
Hawa ni washambuliaji wawili ambao leo watakuwa wakicheza dhidi ya vilabu vyao vya zamani. Kiiza alikuwa Yanga kwasasa yupo Simba wakati Tambwe alikuwa Simba na sasa yupo Yanga na wote kwa pamoja wamekuwa na moto wa ajabu katika kutupia kambani msimu huu.
Kiiza
Mpaka sasa anaongoza kwa kutupia nyavuni akiwa amefunga bao tano baada ya kufunga kwenye mechi ya kwanza bao moja, mechi ya pili bao moja na mechi ya tatu bao tatu na hii ikiwa ni hat-trick ya kwanza kwa msimu huu lakini ikiwa ni hat-trick yake ya kwanza pia akiwa Msimbazi.
Tambwe
Amefunga jumla ya bao tatu hadi sasa. Alifunga bao moja kwenye mechi ya kwanza, halafu mechi ya tatu akatupia mbili dhidi ya JKT Ruvu wakati Yanga ilipoibuka na ushindi wa goli 4-1.
Mtiririko wa matokeo
Yanga
Walianza kwa ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Coasta Union, wakapata ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons na mechi ya tatu wakashinda kwa goli 4-1 dhidi ya JKT Ruvu. Leo wanakutana na ‘mnyama’ hii ina maana kama wanaendelea kwa mfululizo huo wataibuka na goli tano.
Simba
Walianza kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya African Sports kwenye mechi ya kwanza, mechi ya pili wakashinda kwa goli 2-0 dhidi ya Mgambo JKT na mechi ya tatu wakaibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Kagera Sugar. Kama wataendelea na mfululizo huohuo inamaana leo watafunga bao nne.
Magoli ya kufungwa
Kila timu imeruhusu goli moja kwenye mchezo wake wa tatu, timu zote zimefungwa kwenye uwanja wa taifa ambao zinautumia kama uwanja wao wa nyumbani na kila timu imefungwa kwenye mchezo iliopata ushindi mkubwa.
Yanga
 Imefungwa goli moja wakati ilioibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya JKT Ruvu mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa taifa. Yanga wamefunga magoli tisa kwenye mechi tatu walizocheza.
Simba
Ilifungwa goli moja kwenye ushindi wake mkubwa msimu huu hadi sasa ilipoifunga Kagera Sugar kwa goli 3-1 kwenye uwanja wa taifa wakati wao wakiwa wamefunga jumla ya magoli sita hadi sasa.
Historia ya timu hizo kwenye mchezo wa Dar es Salaam Derby
Timu hizi tayari zimekutana mara 79 kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara, mchezo wa leo utakuwa ni wa 80 huku ukiwa ni wakwanza kwenye msimu huu wa 2015/16.
Takwimu zinazungumaje?
Mabinwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Yanga wanaongoza kwa kuwafunga watani zao Simba wakiwa wameshinda mechi 29 kati ya 79 wakati Simba wao wameifunga Yanga kwenye mechi 23 kati ya 79 huku mechi mechi 27 kati ya 79 zikiwa nisare.
Matokeo ya msimu uliopita
Kwenye mechi ya kwanza msimu uliopita timu hizo zilitoka sare lakini mechi ya pili (marudiano) Simba iliitandika Yanga kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wa Uganda Emanuel Okwi.
Maswali mawili ya kujiuliza kabla ya mchezo wa leo
1. Je, Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara watalipa kisasi cha kufungwa mara kwa mara siku za hivi karibuni au Simba wataendelea kupeleka kilio Jangwani?
2. Je, ni nani kati ya Kiiza na Tambwe atakaepeleka kilio kwenye timu yake ya zamani?

Read More »
We need your favorite Opinion! Just give us your Comment below please!

ARSENAL WENGER KAMPA TALAKA MKE WAKE…NA PIA ALIWAHI KUWA NA MCHEPUKO HUU

0 comments
wenger
Watu maarufu kwenye michezo pia wana maisha yao binafsi na wengine huwa hawapendi sana yazungumziwe kwenye media. Lakini kuna gazeti moja la The Sun, kazi yake kubwa ni kutafuta udaku kuhusu michezo na sio matokeo ya mechi peke yake.
Habari kubwa kwa sasa ni kwamba Arsene Wenger anategemea kumpa talaka mke wake Annie Wenger ambae walifunga ndoa mwaka 2010 na kufanikiwa kupata mtoto wa kike.
Lakini taarifa hiyo inasema kwamba Wenger bado atakua anampa support ya kipesa mwanamke huyu na wameshakubaliana kugawana mali zao.
Licha ya kuwa na mtoto wa kike mwenye miaka 18 lakini inasemakana kwamba wapenzi hao(Arsene na Annie) hawakua na furaha kwenye maisha yao ya mapenzi.
Pia inasemekana kwamba wiki chache kabla ya ndoa yao Arsene Wenger alikua na uhusiano wa siri na msanii mmoja wa kike huko Ufaransa anaitwa Sonia Tatar. Kuachana kwao kumethibitishwa na mahakama za Ufaransa na sasa hivi kila mtu anaweza kuwa na uhusiano na mtu mwingine licha ya Wenger kuendelea kuwa na majukumu ya kulea familia yake hasa mtoto wake.
2CA9E99C00000578-3245488-image-m-47_1442974258840
Sonia Tatar.

Read More »
We need your favorite Opinion! Just give us your Comment below please!

Stori ya Mesut Ozil kuihama Arsenal mda wowote ipo hapa

0 comments
Stori za kiungo wa kimataifa wa kijerumani mwenye asili ya kituruki Mesut Ozil kutaka kuihama klabu ya Arsenal zinazidi kuchukua nafasi katika magazeti mbalimbali ya michezo nchini Uingereza. Ozil anaripotiwa kuwa katika mipango ya klabu ya Fenerbahce ya Uturuki.
Stori zilizoandikwa september 24 ni kuwa, klabu ya Arsenal ipo katika mbio za kumshawishi Mesut Ozil aongeze mkataba mpya kabla ya usajili wa dirisha dogo kuanza. Mesut Ozil alijiunga na klabu ya Arsenal mwaka 2013 akitokea klabu ya Real Madrid ya Hispania, kwa ada ya uhamisho wa rekodi wa klabu hiyo wa pound milioni 42.5.
36204
Mesut Ozil ambaye ana miaka 26 aliwahi kutamba katika vilabu vya Schalke 04Werder Bremen, Real Madrid na sasa anakitumikia kikosi cha Arsenal ila klabu hiyo ina hofu huenda kiungo huyo akatimkia klabu ya Fenerbahce ya Uturuki. Mesut Ozil ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa katika klabu ya Arsenal, analipwa pound 140000/= kwa wiki.

Read More »
We need your favorite Opinion! Just give us your Comment below please!

Shabiki wa Timu ya Simba ikufikie hii, na wewe unashiriki kumpata mchezaji Bora wa Mwezi..

0 comments


Ikiwa ni katika muendelezo na harakati za kuipeleka klabu ya soka ya Simba katika mfumo wa kisasa na kujenga kikosi chenye wachezaji wenye morali uwanjani, mwezi September klabu ya Simba imetangaza kuanzisha mfumo wa kumtafuta mchezaji bora wa mwezi.
Kupitia kwa Rais wa klabu hiyo Evans Aveva ametangaza kuanzisha mpango huo mwezi September, ambapo mfumo utakaotumika kumpata mchezaji bora wa mwezi ni mashabiki ndio watakuwa na nafasi ya kumchagua kwa kumpigia kura kwa njia ya sms.
“wanachama na wapenzi wa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji katika kuifanya timu yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni jambo la busara kuwa klabu ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Tunaamini kuwa Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza morali na kujituma kwa wachezaji wetu” >>> Evans Aveva
DAKA RATIBA -02_2

Read More »
We need your favorite Opinion! Just give us your Comment below please!