KIIZA AITUMIA SALAMU YANGA…
FOR ADULT VIDEOS ONLY PRESS BELOW 19++

Hamisi
Kiiza (katikati) akishangilia goli la kwanza na wachezaji wenzake wa
Simba kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Kagera Sugar
mchezo ulipogwa kwenye uwanja wa Taifa
Hamis Kiiza ‘Diego’ ameendelea
kufunga kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) baada ya leo
kuifungia Simba magoli magoli yote matatu (hat-trick) kwenye ushindi wa
goli 3-1 walioupata vijana wa Msimbazi kwenye uwanja wa Taifa wakati
wakiwakabili Kagera Sugar kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya ligi hiyo.
Goli la kwanza la Simba
lilifungwa dakika ya 30 kipindi cha kwanza na Kiiza baada ya Awadh Juma
kupiga pasi iliyomkuta Kiiza ambaye moja kwa moja aliukwamisha mpira
wavuni.
Hamisi Kiiza (wapili kutoka kulia) akishanilia na wachezaji wenzake mara baada ya kufunga goli la tatu
Goli hilo lilidumu kwa muda wote
wa kipindi cha kwanza kwani hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Simba
walikuwa mbele kwa goli 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa
Simba kufunga goli la pili mfungaji akiwa ni Hamisi Kiiza aliyefunga
goli hilo dakika ya 46 kipindi cha pili.
Dakika ya 50 kipindi cha pili,
Keneth Masumbuko aliifungia Kagera Sugar goli la pili baada ya mabeki wa
Simba Hassan Isihaka na Justice Majabvi kutegeana kumkaba Masumbuko
ambaye alifunga goli hilo kirahisi.
Wakati muda ukiwa unaelekea
kumalizika, Hamisi Kiiza alifunga goli la tatu katika dakika ya 90 na
kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick msimu huu.
Kwenye mchezo wa leo Simba
walitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini Ibrahim Ajib alipoteza
nafasi nyingi za kufunga ambazo zingeweza kuwapa Simba magoli mengi
mengi zaidi.
Wachezaji wa Simba walioanza:
Peter Manyika, Hassan Isihaka, Mohamed Hussen, Emery Nimuboma, Simon
Serunkuma, Justice Mjabvi, Awadhi Juma, Said Hamisi Juma, Peter
Mwalyanzi, Ibrahim Ajib na Hamis Kizza
Wachezaji wa akiba: Vicent Angban, Hassan Ramadhani, Said Issa, Mwinyi Kazimoto, Pape Abdoulaye Ndaw, Boniface Maganga na Joseph Kimwaga.
Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza:
Agathon Anton, Salum Kanoni, Said Hassan, Ibrahim Job, Deogratius
Julius, George Kavilla, Iddy Kurachi, Laulence Mugia, Mbaraka Yussuph,
Daudi Jumanne, Paul Ngaliyoma 8
Wachezaji wa akiba: Abuu Hashim, Aboubakari Mtilo, Erick Kihaluzi, Babuu Ally, Keneth Masumbuko, Lambele Jarome, Rashid Loshuwa.


0 comments: