KIIZA AFAFANUA MAANA YA STAILI YAKE YA USHANGILIAJI…
FOR ADULT VIDEOS ONLY PRESS BELOW 19++

Hamisi
Kiiza akishangilia goli la na wachezaji wenzake wa Simba alipofunga
wakati timu yake inacheza dhidi ya Kagera Sugar Jumapili kwenye uwanja
wa Taifa
Mshambuliaji wa Simba Hamisi
Kiiza jana alifanikiwa kuweka rekodi kwenye msimu huu wa ligi kwa kuwa
mchezaji wa kwanza kufunga magoli matatu (hat-trick) kwenye mchezo kati
ya Simba dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa Jumapili kwenye uwanja wa
taifa.
Baada ya mchezo huo kumalizika,
mtandao huu ulipata nafasi ya kuzungumza na Kiiza licha ya mchezaji huyo
kuonekana kuwa na haraka ya kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Kikubwa tulichotaka kujua ni siri ya kasi aliyoanza nayo mshambuliaji
huyo raia wa Uganda ambae ameshafunga kwenye mechi zote tatu na jingine
ni kuhusu staili aliyoitumia kushangilia kwenye mchezo dhidi ya Kagera
Sugar.
Shaffihdauda.com:
Kiiza umekuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli matatu ndani ya msimu
huu, nini siri ya mafanikio yako maana mbali na kufunga goli tatu leo
lakini kila mechi umefunga
Hamisi Kiiza: “Tumeshinda kwasababu tumecheza kitimu, tulifanya mazoezi kitimu sifa zote zinaenda kwa timu yangu na sio mimi”.
Shaffihdauda.com:
Umefunga hat-trick leo (jana) mechi ijayo unakutana na Yanga, mchezo
unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu zote mbili. Itakuwa mechi
yako ya kwanza dhidi ya timu yako ya zamani ya Yanga tangu utue Simba,
watu watarajie nini siku hiyo?
Hamisi Kiiza:
“Ni mechi ngumu sana inafaa kujipanga, bado hatujakaa sawa kama vile
tunavyotaka. Tunamuomba Mungu ili tupate matokeo mazuri kwenye mechi
hiyo”.
Shaffihdauda.com: Kila bao ulilofunga ulikuwa unashangilia kwa kuashiria muda, ulikuwa unamaanisha nini kwa kufanya hivyo?
“Namaanisha ligi bado kwahiyo kuna mambo mengine mazuri yanakuja, mashabiki wa Simba waendelee kutupa muda na kuwa na subira”.


0 comments: